CBC: Wanafunzi wa Daraja la 7 Kujiunga na Shule za Kutwa

NAIROBI, KENYA
12th May 2022

Katibu wa Baraza la Mawaziri la Elimu George Magoha, amebadilisha agizo lililoripotiwa kote nchini, linalohusu udahili wa Wanafunzi wa Sekondari ya vijana, chini ya Mtaala unaozingatia Umahiri (CBC).

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Mei tarehe 11, Waziri Mkuu aliagiza kuwa shule zote za upili za kutwa na za bweni zitapokea wanafunzi wanaoingia katika Shule ya Sekondari ya Vijana.

Aidha alibainisha kuwa, wizara imetenga shule za msingi zipatazo 1,500 ambazo zitakuwa na wanafunzi wanaoenda darasa la saba.

mabadiliko haya yataathiri kundi la kwanza la wanafunzi wa CBC wanaotoka Darasa la 6 kwenda la 7 mwaka wa 2023.

“Wizara imebaini shule za msingi 1,500 ambazo zitakuwa na shule za sekondari za chini kwa sababu zina vifaa vya kutosha vya kujifunzia na kufundishia na nafasi kubwa za ardhi kwa ajili ya upanuzi,” taarifa hiyo ilisema.

Agizo hilo linakuja baada ya ripoti kuenea kuwa wizara ilikuwa tayari kudahili wanafunzi wote wa darasa la 7 katika shule za sekondari za kutwa.

Naibu Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari Lawrence Karundi amesema kuwa wanafunzi wataishi katika shule za kutwa zilizo karibu nao huku serikali ikitatua changamoto ya nafasi ya mabweni.

Swali la nafasi linachangiwa na ukweli kwamba wanafunzi wa sasa wa Darasa la 8 pia wanaingia shule ya upili chini ya mtaala wa zamani. 

“Linapokuja suala la mabweni, hasa ya sekondari ya chini, sisi tunachozingatia ni kwamba hii iwe shule ya kutwa, siyo ya bweni” Karundi alinena.

Hofu hii pia ilikuja baada ya wazazi kulalamika kwamba, watoto hawa wanaomaliza darasa la sita, bado ni wadogo mno na hawawezi kujiangalia vizuri wala kujihimili, na hivyo kupendelea shule ya kutwa.

Wanafunzi hao  watawekwa katika Shule za Sekondari za Vijana, ambazo zitalingana na ufaulu wao, masomo waliyochagua na uwezo wa kujiunga na shule za kutwa.

Watahiniwa hao  watajaribiwa katika masomo matano,  yakiwemo Hisabati, Kiingereza, Kiswahili, Sayansi Jumuishi na Sayansi ya Ubunifu na Jamii.

Mwandishi-Khadija Mbesa

Advertisement

One thought on “CBC: Wanafunzi wa Daraja la 7 Kujiunga na Shule za Kutwa

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Website Powered by WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: