kesi baina ya Wazazi wawili juu ya utunzaji wa Mtoto.

By Khadija Mbesa

Mara nyingi waachanapo wazazi wawili na kujitoa kwenye ndoa yao basi mtoto ndie huumia haswa. Katika hii kesi iliyotokea mwingi ambapo, mama anamshitaki baba wa mtoto wake kwa madai ya kumdhalilisha mwanawe  huku akiomba korti iweze kumpatia ulinzi wa mwanawe. Hii ikimaanisha kuwa mtoto asiendelee kuishi na babake kama hapo awali, bali mtoto huyu aanze kuishi na mamake.

Mama huyo kwa jina la Josephine Kanini Kawila akimshtaki Eric Munyaga Muthoka, baba ya mtoto wao ambaye ni Sarah Wambui mwenye miaka 9 na akiwa bado darasa la nne.

Wazazi hao wawili walikua ndani ya ndoa, wakatalikiana na kila mzazi akaingia kwa ndoa ingine.

Baada ya Mashtaka hayo Eric Munyaga alilazimishwa kumpeleka Sarah Wambui kortini tarehe 9 mwaka wa 2020, huku akifuatana na askari kutoka kituo cha polisi cha mwingi. hati ya kukamatwa  kutolewa hadi tarehe 9 Januari 2020 ikifuata ukamili wa maagizo.

Kesi hii ilipelekwa kwa afisa wa watoto, Francis Katuku ambae alianza kuishughulikia haraka iwezekanavyo. Sarah aliweza kumwambia afisa huyo anataka kumwelezea mamake jinsi alivyomkwaza sana, ila hakuweza kusema kitu chochote kwa sababu ya uwepo wa babake.

Mama Sarah alisema ya Kwamba kuachana kwake na baba mtoto ni kwa sababu ya Vurugu baina ya Wazazi wa Bwana na yeye ambapo ilimlazimu kutoka kwa hiyo ndoa, na kumwacha Sarah kwa dadake, Na ndio wakati huo baba Sarah aliona mpenyo wa kumchukuwa mwanawe kutoka kwa dada ya Mama Sarah. Katika juhudu zote za kutaka kupewa mtoto wake mama Sarah alienda juu chini, huu ukiwa wakati mgumu sana kwani madai yake yalitupiliwa mbali, hii ni kwanzia mwaka wa 2017.

Mama Sarah alidai ya kwamba, Eric Muyanga, alikataa katukatu kumwambia kitu chochote kuhusu mwanawe na pia alikataa kumwambia anapoishi.

korti ilimuamrisha Afisa Kituku kuenda kwa nyumba ya mshtakiwa ili kuangalia kama ni kweli huyo mtoto alikuwa ananyanyaswa. Bali alikuta mtoto huyo ako kwa Afya nzuri na analelewa ipasavyo na nyanyake pamoja na babake. Sarah alikuwa anaenda shule na hakuwa ndani ya hatari yeyote.

Na kwa hilo korti imetoa amri ya kwamba Sarah ataendelea kuishi na babake kama hapo awali, na ataendelea kwenda shule ile ile aliyokuwa anasomea, pia alitoa amri ya kwamba, Mama Sarah anaweza kwenda kumuona mtoto wake muda wowote.

kesi nyingi mno kenya hii zimeibuka za upiganaji wa kung’ang’ania ulinzi na utunzaji wa watoto baina ya wazazi wawili,  Haya yanaongezewa sana na talaka kati ya wazazi hao. Bila wao kujua wanamkwaza na kumdhalilisha mtoto huyo akiwa bado mdogo.

Follow us on Twitter: https://twitter.com/mtotonews

Subscribe to our YouTube Channel: http://youtube.com/mtotonewstv

Mtoto News is a Digital Online platform of news, information, and resources that aims at making significant changes in the lives of children by making them visible. Read mtotonews.com or follow us on Twitter and Facebook @mtotonewsblog 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Powered by WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: