ukeketaji,Dhulma kwa mtoto wa kike

by Khadija Mbesa

Ukeketaji ni tohara au kutahiriwa.

Ukeketaji  ni utaratibu ambapo viungo vya siri vya wanawake hujeruhiwa na hubadilishwa, ila hakuna sababu za kimatibabu katika tendo hili. Jambo hili linaweza kuathiri sana afya ya mtoto wa kike katika maisha yake ya baadae. Watoto wengine hufariki kutokana na kupoteza damu au kuathirika kwa kusambazwa magonjwa kutokana na utaratibu huu.

Ukeketaji wa  umekithiri kaskazini mashariki, (kaskazini mashariki ni maeneo ya garissa, wajir, ijara na mandera), ambapo mtoto yeyote wa kike anapaswa kukeketwa baada ya kuvunja ungo/baleghe.

mabinti

Kupitia utafiti wa serikali na hata shirika la UNICEF, matokeo yao yanaashiria kuna mbinu za kisasa za ukeketaji,ambazo unakuta mtoto mdogo, tuseme wa umri wa miaka mitatu-mitano hukeketwa na mapema. Kisha kwenye matokeo yayo hayo pia waligundua kuna maafisa wa matibabu wanaotumiwa kutekeleza tohara ya kina dada.

Kwa nini nazungumzia swala la ukeketaji? kwa sababu lipo na linaendelea katika jamii tunamoishi, unaona familia inamsafirisha msichana kutoka ughaibuni hadi kenya kwa ajili ya kukeketwa. Huu ndio uozo unafaa tuupinge kwa namna yoyote ile ili kunusu maisha ya mtoto wa kike ya usoni.

Tupige vita ukeketaji ili kumnasua mtoto wa kike. Hili suala halijaaza leo wala jana, huu mjadala umekua ukiongelewa mara kwa mara mitandaoni,magazetini na pia vitabuni, ila watu wamejieka sikio la kufa na watoto wengi wa kike wameathirika kwa sababu ya jamii kujitia hamnazo kuhusu hili suala.

no

Kwa nini Ukeketaji hufanywa?

Wazazi wa mschana au ndugu na jamaa zake hufanya mipango ili yeye akeketwe, kisa na maana ni;

  • Desturi, kwani familia nyingi kaskazini mashariki zinadai kuwa, mtoto wa kike akifanyiwa tohara basi hutulia.
  • Kuhifadhi utamaduni, kuendeleza mila yao.
  • Kuhifadhi ubikra,
  • Kukubalika katika jamii, haswa kuhusiana na maswala ya ndoa.

Sababu hizi zimejengwa na kutokua na ufahamu katika jamii au kutoka na elimu ya kutosha.

Ukeketaji ni kinyume cha sheria.

Kukeketwa kwa watoto ni lazima usitendwe kamwe hapa nchini pia nje ya nchi.

Pia ni kinyume cha sharia kumsaidia mtu kufanya tendo hilo la ukeketaji kwani una madhara mengi kama vile,

  • Kutokwa damu nyingi, majipu na uvimbe katika sehemu za siri za mtoto.
  • Magonjwa ya kuambukizwa mara kwa mara ambayo inaeza fanya mtoto wa kike kutoweza kujifungua/kua tasa katika maisha yake ya baadae.
  • Matatizo wakati wa kukojoa. Hii inaeza chukua miezi ya kupona.
  • Matatizo ya uzazi, kwani inakua shida sana kujifungua inaeza sababisha hadi kifo. Athari kuhusu usalama wa mzazi na mtoto ni sawa na kuekwa kwenye mizani ya uhai, ni aidha mmoja afe, mwengine aishi ama wote wafe/wote waishi. Na inapofikia hapa basi jamii ni kama inamkatia mtu maisha ya baadae pale inapofikiria ukeketaji.
  • Maumivu yasiyopungua, maumivu yanaeza endelea kwa wiki ama hata miezi.

images

huku ni kumnyima haki mtoto wa kike ya viwiliwili vyake, ndoa za mapema, kumkatiza ari ya kusoma maishani wakati siku za usoni hatakua na Imani ya uajibikaji na majukumu yake maishani.

tuipinge hii tohara ya wasichana na wanawake katika jamii tunamoishi.Unapoona matokeo yakiashiria upungufu wa asilimia ishirini na moja, basi tujizatiti na kuendelea kupinga uovu huu katika karne ya leo. Wazazi hawafai kamwe kuwapeleka watoto wao kukeketwa. Mtoto ana haki ya kuheshimiwa viwiliwili vyake pasi kusukumwa,iwe wajibu.

#ukeketaji

Picha kwa hisani;

Follow us on twitter: https://twitter.com/mtotonews

Subscribe to our YouTube channel: https://youtube.com/mtotonewstv

Mtoto News is a digital online platform of news,information, and resources that aims at making a significant change in the lives of children by making them visible.

Read mtotonews.com or follow us on twitter and facebook @mtotonewsblog

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Powered by WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: